KOCHA
David Moyes amesema kwamba Wayne Rooney hatauzwa na Manchester United
na hili ni sawa na pigo lingine kwa Arsenal, ambayo ilikuwa inamtaka
mchezaji huyo.
Kocha
huyo mpya wa Old Trafford amekutana na Waandishi wa Habari leo kwa mara
ya kwanza tangu athibitishwe kuwa mrithi wa Sir Alex Ferguson, kiasi
cha miezi miwili iliyopita na akakutana na maswali kibao kuhusu
mustakabali wa mshambuliaji huyo wa England.
Moyes
amethibitisha kwamba Rooney – ambaye inafahamika alimuambia Ferguson
anataka kuondoka– amebadilisha mawazo yake na amesema atabaki klabuni
Karibu kwenye bodi: David Moyes amefanya Mkutano wake wa kwanza na Waandishi wa Habari kama kocha wa Manchester United
"Wayne hauzwi," amesema. "Ni mchezaji wa Manchester United na atabakia kuwa mchezaji wa Manchester United,".
"Tumezungumza
mara kadhaa. Vyovyo ilivyotokea kabla, na Wayne tunafanya kazi pamoja
sasa. Nimeona nuru katika macho yake, anaonekana mwenye furaha na kama
anayekwenda kukita chini. Nasonga mbele kufanya naye kaziI na hatauzwa.
"Kulikuwa
kuna kikao cha faragha baina ya Wayne na Sir Alex. Nasona sasa. Sijui
kilichozungumzwa katika kikao chao cha faragha. Kama ninavyosema,
nasonga mbele katika kumuweka Wayne Rooney katika kiwango
sahihi,"alisema.
Yameisha: Sakata la Rooney linaonekana kufikia tamati baada ya Moyes kusema mshambuliaji huyo hatauzwa
Moyes, mwenye umri wa miaka 50, amejiunga na United kwa Mkataba wa miaka sita baada ya kuitumikia kwa miaka 11 Everton.
Moyes akiwa ofisi mpya, Old Trafford anaonekana mwenye furaha
0 comments:
Post a Comment