AJAX FOOTBALL ACADEMY INAJIVUNIA KIZAZI HIKI CHA DHAHABU.
patrick Kluivert
huyu jamaa alizaliwa mwaka 1976 na kulelewa kisoka na Ajax ya huko kwao Uholanzi.ni moja kati ya watu waliojaaliwa kujua goli lilipo.alikuwa na nguvu na urefu wa kutosha,kitu kinachonifanya niseme yeye ndiye mchezaji wangu bora wa magoli ya vichwa.
Edgar Davis
huyu ni kiungo mkabaji kazaliwa 1973.amekulia pia Ajax fc.nadhani Arturo Vidal ndo kidogo naweza sema ni mbadala wake kwenye dimba la chini.Davis wengi wanamjua kama "mzee wa miwani" jamaa alikuwa mkorofi sana ingawa aliujua mpira.i miss you Davis.
Denis Bergkamp
mholanzi aliyezaliwa 1969 na kuinuliwa na club ya Ajax ni bonge moja la kiungo mshambuliaji kuwahi tokea Duniani.pale katika uwanja wa Emirates kuna sanamu yake.kabla ya Kluivert kuja juu,yeye ndiye alikuwa mfunga bora wa uholanzi wa muda wote.
Clarence Seedorf
club ya ajax inastahili pongezi,huyu nae wao ndo walimkuza na kumuibua Duniani amezaliwa 1976.ananguvu na kasi ya hatari,anapiga mashuti ni balaa.nadhani kwa sasa anamalizia ufundi wake kule Brazil samba ilikozaliwa.
Edwine Van Der sar
amezaliwa mwaka 1970 na yeye ametoka pale Ajax FC.anajua sana kulinda goli lake.ameokoa sana michomo ya penalty.huyu ndo aliacha mzimu pale OT uliomsumbua De Gea msimu wake wa kwanza.anamtoto wake wa kiume ambaye nae ni goli kipa kwenye timu ya chini ya miaka 12 pale manchester united.
0 comments:
Post a Comment