mourinho hoi pale BERNABEU
Ukimuangalia kwa jicho la kinazi utagundua kwamba Mourinho huwa hashindwi,anafanya chochote uwanjani,hasumbuliwi na wachezaji wala utawala wa club.
Lakini ukimuangalia kwa jicho la soka,utagundua kwamba Real Madrid imemshinda.kwanza mbinu yake ya kukaba na kushambulia kiujanja ujanja pale imekatalia.anasifika kwa kuwasifia wachezaji wake lakini Madrid anawaponda tu kila siku.
Kote alikopita alikusanya vikombe kama njugu,pale kaokoteza tu.Na badala ya kuendeleza ufalme wa madrid La Liga,yeye kachezea vichapo kibao toka kwa Barcelona hasa PEP GAUDIOLA.
Nadhani siku zake za "special one" zinahesabika,miyangu macho tu.
0 comments:
Post a Comment