HAWA HUWA HAWAONGEZEKI KIWANGO
Theo walcott
tangu anunuliwe toka southampton huyu dogo alikuwa balaa uwanjani na sifa kubwa sana ya Theo,ni mbio.wakati ananunuliwa wenger aliamini ndo mbadala wa Thierry Henry kwa namna alivyokuwa na speed na uwezo wa kufunga,lakini nimuonavyo kwa sasa sidhani kama atamfikia TITI.
Luis Nani
Mreno huyu anafanana kiasi flani na Christiano Ronaldo.anambio,chenga na akili ya kufunga pia.anacheza winga kama ilivyo kwa CR7.wakati CR7 anaondoka united,wengi tuliamini NANI yupo wa kuziba nafasi hiyo lakini kwanavyomuona siku hizi,sidhani kama atafika hata nusu ya CR7.
Shaun wright Phillips
huyu ni muingereza mwingine ambae anakimbia sana uwanjani.kacheza chelsea,City na sasa yupo kwenye timu yangu QPR.yeye anachojali ni mbio na kupiga chenga hata kama anatoka nje ya uwanja,hana habari.yuko tayari kumpiga mtu tobo,hata kama mpira kipa atadaka.sasa hii akili au matope?
Aaron Lenon
baada ya club ya Leeds kufilisika,alinunuliwa pale White Hart Lane.anapenda sana kukimbia uwanjani hata kama hajui anakokwenda.yaani hawa waingereza kama wamerogwa.Alipotua Spurs misimu miwili mfululizo alitajwa kugombea kwenye PFA mchezaji chipukizi na Ronaldo na Rooney wakamshinda lakini huku anakokwenda siku hizi,itakuwa ngumu kuwepo hata kwenye kikosi cha PFA cha msimu.
0 comments:
Post a Comment