HII YAWEZA KUINUSURU ARSENAL
Beki namba 2 Bakari Sagna anatakiwa kupewa msadidizi bila kujali anaondoka ama anabaki emirates.Sagna jua limeanza kuzama na kumng'ang'ania ni kujidanganya.haaminiki kwenye kukaba na hata anapopanda,mara nyingi hutoa crosi pumba.Lukasz Piszczek anahitajika.
Katika ushambuliaji,hamna kitu.usiwaamini Gervinho,Giroud,Theo wala Podolski.nadhani mtu kama Rooney au Mario Gomes wanaweza kutatua tatizo hili pale Emirates.
Dimba la chini nadhani sio tatizo kwa sababu Arteta ameonyesha kumudu ingawa nae umri anaanza kumkimbiza dimbani.wakipata mtu kama Arturo Vidal au aina ya Mikel Obi,Dimba litakuwa la uhakika.
Beki ya Gibbs na Nacho Monreal kama siielewi hivi nadhani sijapata muda wa kutosha wa mumfuatilia Nacho ila kwa Gibbs,mmmh utata mtupu!!.kwa muda ambao Nacho kacheza na Arsenal,ameonekana ni beki wa kawaida tu.
Viungo hawahitajiki,wamejaa mpaka wanamwagika.Kama Fabianski,Vito Manoni na Wojoh Seszcszney wote wataendelea kuwepo,sioni kama wenger anahitaji kununua kipa mwingine.
Chamakh na Giroud wazuri sana kwenye mipira ya vichwa ila miguuni,hawana shabaha.
0 comments:
Post a Comment