PATA VOCHA KWA KUTABIRI MATOKEO SIMBA VS YANGA
Watu wengi wanashindwa kuelewa kwamba refa na wasaidizi wake ni binadamu na ni mashabiki wa soka.Tanzania kama mtu asipokuwa YANGA basi atakuwa SIMBA kwahiyo hata refa atakuwa ama SIMBA au YANGA lakini hii sio tiketi ya yeye kupendelea upande mmoja na sisi kama mashabiki tusiwe na wasiwasi kwa maamuzi yoyote hasa ya utata kwa sababu hata ulaya marefa wanakosea.
Mchezaji anaweza kosa goli la wazi na hatumpi sana lawama ila refa asipoona offside moja,magazeti na vyombo vyote vya HABARI vitamzonga.lazima tujue mchezo wa mpira ni mchezo wa makosa.Najua timu zimejiandaa vya kutosha na waganga najua washakula chao,nategemea kuona mchezo wa leo kuwa wa kasi na ushinda huku pande zote zikionyesha soka safi.
YANGA anakwenda kwenye mchezo huu akiwa anapewa nafasi kubwa ya kushinda kufuatiwa kuwa na wachezaji wengi wenyeuwezo mkubwa na uzooefu.Simba inatumia vijana wake ambao nao wanauwezo mkubwa ingawa wanakosa uzoefu hususani wa mechi ya watani wa jadi.Hii sio sababu ya kuwafanya wapoteze mchezo huu.vijana wa SIMBA watataka kutumia nafasi hii kuwaaminisha viongozi na mashabiki kwamba wameiva na wako tayari kwa chochote kwa kumfunga YANGA leo.
MCHEZO HUU utarushwa na kituo cha supersport kwa hiyo nadhani ni nafasi kwa wachezaji wetu kuonyesha kandanda safi na lakuvutia,natarajia kuona fair play na mchezo wa kuingwana.kuvunjana miguu,vipepsi na ghasia nyingine uwanjani zimepitwa na wakati.Tusijifanye kwamba sisi ndiyo tuna DERBY pekee hapa ulimwenguni hata UNITED vs CITY huwa wanainuana uwanjani LIVERPOOL vs EVERTON huwa hawavunjani miguu uwanjani.MADRID alikula tano toka kwa BARCA lakini wote walionyesha mchezo wa kiungwana.
kutoka mfukoni kwangu,nitatoa vocha ya ELFU MBILI kwa mtu mmoja wa kwanza kutabiri kwa usahihi matokeo ya mechi hii kabla haijaanza.nitakuwepo UWANJANI LEO na baada ya mechi nitarudi kufanya uchambuzi wa kile nitakachoona.
0 comments:
Post a Comment