Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 January 2015
Tuesday, January 27, 2015

Van persie hatihati kubaki Manchester.



Na Chikoti Cico


Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Robin van Persie ameonyesha wasiwasi kama atasaini mkataba mpya na klabu hiyo wakati mkataba wake utakapoisha ndani ya miezi 18.

Mshambuliaji huyo ambaye alihamia mwaka 2012 klabu ya Manchester akitokea klabu ya Arsenal kwa ada ya pauni milioni 24 na kuifungia timu hiyo magoli 26 huku akiiwezesha kunyakua kombe la ligi amekubali kwamba amekuwa mbovu kwenye msimu huu wa ligi.

“Mwaka huu nimecheza kitu kama michezo 20 na nimefunga magoli manane-sina furaha na hilo, nataka kufunga zaidi nitafanya kila kitu, kila siku mazoezini na wakati wa mecho nitaendelea kufanya kile ambacho nimekuwa nikikifanya kwa miaka 10 iliyopita kufanya hayo magoli” alisema Van Persie.

Van Persie ambaye atatimiza miaka 32 mwezi Agasti mwaka huu mkataba wake unatarajiwa kuisha wakati wa kipindi cha majira ya joto ya mwaka 2016. 

Wakati huo huo United bado hawajaanza kuongelea kuhusu mkataba mpya swala ambalo mchezaji huyo amesema liko nje ya uwezo wake.

“Sio swala kuhusu mimi, kwasasa ninakaa hapa kwa miezi 18, ndivyo ilivyo hakika, siwezi kuangalia mbeleni, sijui nini kitakachotokea baada ya hilo, inabidi tusubiri na tuone” alisema Van Persie.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!