Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 January 2015
Tuesday, January 27, 2015

Real Madrid kufungiwa kama Barcelona.



Na Chikoti Cico

Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania inaweza kufungiwa kufanya usajili kama ilivyotokea kwa klabu ya Barcelona baada ya shirikisho la soka duniani FIFA kufungua upelelezi dhidi ya usajili wa wachezaji wenye umri mdogo kwenye klabu hiyo.

Upelelezi wa FIFA dhidi ya Real Madrid umelenga kwa wachezaji wawili wenye umri wa miaka 12 walionunuliwa na klabu hiyo kutoka Venezuela mwaka 2012, Manuel Godoy na Ferndando walikuwa kwenye safari za majaribio na klabu kubwa lakini kabla hawajafika River Plate na Milan, Madrid waliwanyakua kupitia mtu wa katikati ambaye ana shule ya soka kwenye mji mkuu wa Hispania.

Wa kwanza alisajiliwa na Madrid mwaka 2012 na wa pili alisajiliwa akiwa na miaka 14 mwaka 2013 ambaye kwasasa yuko kwenye mfumo wa vijana wa klabu ya Rayo Vallecano.

Madrid wana mwezi mmoja wa kuwasilisha nyaraka muhimu kwa FIFA kuonyesha kwamba hawajavunja kifunga cha 14 cha mamlaka hayo ya soka ambacho kinaruhusu kusajiliwa kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 18 kutoka nje ya Muungano wa nchi za Ulaya (EU) kama wazazi wa mchezaji huyo walitakiwa kuhamia kwenye nchi ambayo klabu hiyo inatoka kwasababu ambazo sio za kimpira”

Sheria hiyo ipo kwaajili ya kuvizuia vilabu kuwafanyia makazi familia kutoka nchi ambazo hazipo ndani ya EU ili kuweza kuwasajili wachezaji wadogo kutoka kwenye familia hizo.

Mwishoni mwa mwaka uliopita klabu ya Barcelona ilikutwa na hatia ya kusajili wachezaji wenye umri mdogo kitendo kilichopelekea FIFA kuifungia klabu hiyo kusajili kwa mwaka mzima wa 2015 huku wakitakiwa kulipa faini ya kiasi cha dola 293,000.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!