Searching...
Image and video hosting by TinyPic
22 January 2015
Thursday, January 22, 2015

Manchester United kuongeza 'majembe' dhidi ya CambridgeNa Florence George


Mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi na Manchester United Robin Van Persie anatarajiwa kurudi uwanjani siku ya Ijumaa katika mechi ya kombe la FA dhidi ya Cambridge.


Akiongea na waandishi wa habari, kocha wa timu hiyo Louis Van Gaal alisema kuwa mchezaji huyo atakuwepo uwanjani baada ya  kupona majeraha yake ya kifundo cha mguu huku Luke Shaw naye akitarajiwa kurejea uwanjani siku hiyo.

Van Persie aliyefunga magoli nane hadi sasa alikosekana katika mechi dhidi ya QPR ambapo timu yake iliibuka na ushindi wa magoli 2-0 huku Radamel Falcao na Angel Di Maria wakiongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

Kuelekea mchezo huo Manchester United itaendelea kuwakosa mabeki wake Cris Smalling na Jonny Evans huku Ashley Young akiendelea kuwa nje kwa muda wa mwezi mmoja zaidi.

 Goli kipa Victor Valdes ,aliyejiunga na timu hiyo mapema mwezi huu baada ya kufanya mazoezi na timu hiyo kwa muda wa wiki 10 anatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Cambridge japo Van Gaal amegoma kufafanunua kuhusu habari hiyo.


 

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!