Searching...
Image and video hosting by TinyPic
22 January 2015
Thursday, January 22, 2015

Wakala wa De Bruyne azigomea Bayern Munich,Manchester United na Arsenal







Na Florence George


Patrick De Koster ambaye ni wakala wa mchezaji wa Wolfsburg, Kevin de Bruyne amesema kuwa mchezaji huyo hawezi kuuzwa kwenda klabu nyingine katika kipindi hiki cha usajili.


Kevin de Bruyne alijiunga na Wolfsburg ya nchini Ujerumani akitokea klabu ya Chelsea msimu uliopita kwa kiasi cha Euro 18 na alifanikiwa kuanza michezo sita tu alipokuwa Chelsea.

Mchezaji huyo mwenye Umri wa miaka 23 amefanikiwa kuisadia timu yake msimu huu ambapo hadi sasa Wolfsburg wanashika nafasi ya pili nyuma ya Bayern Munich huku akifunga magoli sita na kusaidia upatikanaji wa magoli 12(assists).

Mbeligiji huyo amekuwa akihusishwa kuhitajika na klabu za Bayern Munich,Manchester United na Arsenal lakini wakala wake amesisitiza kuwa mchezaji huyo hawezi kuuzwa kokote kule katika kipindi hiki.

Akiongea na Gazeti la michezo la Guardian, De Koster alisema kuwa mchezaji huyo anafuraha katika timu hiyo baada ya kuwa na kipindi kigumu katika klabu ya Chelsea na alikuwa akihitaji kucheza mechi nyingi kitu anachokipata katika klabu hiyo kwa sasa hivyo hafikirii kuachana na timu hiyo.

De Bruyne alihudhuluria mazishi za mchezaji wenzake wa klabu hiyo Junior Malanda siku ya Jumanne aliyefariki katika ajari ya gari mapema mwezi huu, wachezaji hao walikuwa wanacheza pamoja katika timu ya taifa ya Ubeligiji.


 




0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!