Searching...
Image and video hosting by TinyPic
23 January 2015
Friday, January 23, 2015

Tunisia yaichapa Zambia AFCON





Na Chikot Cico


Michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika imeendelea kushika kasi nchini Guinea ya Ikweta ambapo katika mchezo wa kundi B kati ya Tunisia dhidi ya Zambia uliochezwa jana uliisha kwa Tunisia kushinda kwa magoli 2-1 na kufikisha alama nne.
 
Magoli yaliyofungwa na Ahmed Akaichi na Yasine Chikhaoui kwenye dakika ya 70 na 89 ya mchezo yaliipa Tunisia ushindi huo huku goli la kufutia la machozi la Zambia likifungwa na Emmanuel Mayuka kwenye dakika ya 59 ya mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua.

Kwa matokeo hayo Tunisia kwasasa inaongoza kundi B ikiwa na alama nne huku Visiwa vya Cape Verde na DR Congo wakishika nafasi ya pili na ya tatu wote wakiwa na alama mbili huku Zambia ikishika mkia ikiwa na alama moja.

Mchezo mwingine wa kundi B ulikuwa ni kati ya DR Congo dhidi ya Visiwa vya Cape Verde ambapo mchezo huo uliisha kwa sare ya 0-0 hivyo timu zote mbili kugawana alama moja moja. Wakati huo huo siku ya Jumatatu Tunisia watacheza dhidi ya Congo na Zambia dhidi ya Visiwa vya Cape Verde kumalizia michezo ya hatua ya makundi kwa kundi B.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!