Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 February 2017
Wednesday, February 01, 2017

CHELSEA vs LIVERPOOL HAKUNA MBABE, ARSENAL APIGWA NYUMBANI





Na FLORENCE GR

Klabu ya soka ya chelsea imefanikiwa kuondoka na pointi katika uwanja wa Anfield baada hapo jana usiku kutoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Liverpool ambayo bado haijafanikiwa kushinda mechi ya ligi kuu kwa mwaka huu wa 2017.

Chelsea ndo ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa beki wake wa kati mbrazili David Luiz kwa mpira wa adhabu wa mita 25 katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo lakini liverpool ambao walionyesha kiwango kizuri hiyo walifanikiwa kusawazisha goli hilo kupitia kwa mholanzi Georginio Wijnaldum kwa kichwa dakika ya 11 baada ya kutoka mapumziko.

Liverpool ambao hapo jana walimaliza gundu la kupoteza michezo mitatu mfululizo walionekana kucheza ka kujiamini huku mshambuliaji wa Roberto Firnino akikosa nafasi mbili za wazi  moja akipaisha mpira juu ya lango huku nyingine ikienda moja kwa moja mikononi mwa Thibaut Courtois katika dakika za mwishoni.

Zikiwa zimebaki dakika 14 kabla mchezo haujamaliza chelsea walipata mkwaju wa penati baada ya Diego Costa kuangusha ndani ya eneo la hatari na Joel Matip lakini penati hiyo iliyopigwa na Costa iliokolewa vizuri na Simon Mignolet hivyo kusaidia liverpool kuondoka na pointi moja.

Katika mchezo mwingine uliopigwa katika dimba la Emirates ulishuhudiwa timu ya Watford ambao imeondokewa na mshambuliaji wao raia wa nigeria Ighalo iliwashangaza wenyeji wao Arsenal kwa kuwafunga magoli 2-1.

Shukrani kwa magoli ya haraka haraka yaliyofungwa na beki wa zamani wa Tottenham Hotspur Younes Kabou dakika ya 10 kabla ya Troy Deeney kufunga goli la pili baada ya kipa wa Arsenal Peter Cech kuokoa shuti la Etienne Capoue dakika ya 13.

Arsenal walirudi kipindi cha pili kwa kasi na kufanikiwa kupata goli kupitia kwa mchezaji wa kimataifa wa Nigeria Alex Iwobi huku kipa wa Watford Heurelho Gomes alifanya kazi ya ziada kuokoa mashuti ya Theo Walcott,Alex Iwobi na Mesut Ozil hivyo hadi mechi inaisha Arsenal akikubali kipigo kutoka kwa watford.

Sunderland ambao wako chini kabisa ya msimamo walitoka sare ya 0-0 dhidi ya Tottenham ambao wapo katika mbio za ubingwa wa EPL.

Spurs ambao katika michezo mitano iliyopita wamefanikiwa kufunga magoli 16 walishindwa kuipenya kabisa ngome ya ulinzi ya Sunderland ambao katika mchezo huo walifanikiwa kupiga mashuti matatu tu langoni mwa spurs huku umiliki wa mpira ukimilikiwa kwa asilimia 73 na totenham lakini mambo bado yalikuwa magumu.

Mabingwa watetezi wa ligi hiyo timu ya Leicester bado wapo katika hali mbaya ambapo walikubali kipigo kigine toka kwa Burnley cha goli 1-0 hivyo kufanya mabingwa hao kushindwa kuibuka na ushindi ugenini katika mchezo wowote ule wa ligi kuu msimu huu huku Burnley ukiwa ni ushindi wa tano mfululizo katika uwanja wa nyumbani.

Mpaka sasa msimamo wa ligi kuu EPL unaonyesha kuwa Chelsea anaongoza ligi hiyo akiwa na pointi 56 akifuatiwa na Totennham mwenye pointi 47 sawa na Arsenal wakiwa wanatofautiana idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa huku nafasi ya nne ikikaliwa na Liverpool yenye pointi 46 huku timu zote hizo zikiwa tayari zimeshacheza mechi 23 mpaka sasa.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!