Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 January 2015
Friday, January 30, 2015

Gerrard na mechi 700 mguuni.


Na Chikoti Cico

Kiungo wa klabu ya Liverpool Steven Gerrard anatarajiwa kuvaa viatu vitakavyokuwa vimenakshiwa na namba “700” kwenye mchezo dhidi ya West Ham utakaopigwa siku ya Jumamosi kwenye uwanja wa Anfield kama kumbukumbu ya michezo 700 atakayofikisha hiyo jumamosi.
Gerrard ambaye anatarajiwa kuiacha klabu ya Liverpool mwishoni mwa msimu huu na kuelekea nchini Marekani kuichezea klabu ya LA Galaxy aliweka picha kwenye mtandao wa Instagram kuonyesha viatu hivyo.
Nahodha huyo wa Liverpool anashika nafasi ya tatu kwenye orodha ya wachezaji walioichezea Liverpool michezo mingi huku akiwa nyuma ya Jamie Carragher ambaye anashika nafasi ya pili akiwa ameichezea Liver michezo 737 na Ian Callaghan ambaye anashika nafasi ya kwanza na michezo 857.
Mpaka sasa Gerrard ameichezea Liverpool michezo 699 ambayo inahusisha michezo 495 ya ligi kuu nchini Uingereza, michezo 40 ya kombe la FA, michezo 30 ya kombe la ligi, michezo 130 ya Ulaya na michezo minne sehemu nyingine.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!