Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 January 2015
Friday, January 30, 2015

Manchester United yapata pigo tena

Na Florence George

Klabu ya soka ya Manchester United imepata pigo baada ya kiungo wake wa kutegemewa Muingereza Michael Carrick kupata majeraha ya misuli na atakuwa nje kwa muda wa wiki nne,hayo yamesemwa na kocha wa timu hiyo Louis Van Gaal katika mkutano na waandishi wa habari hii leo.


Carrick amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha United tangu aliporejea akitokea majeruhi mwezi November na kuisaidia timu yake kushinda michezo sita mfululizo baada ya kuanza vibaya msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 atakosa mchezo wa kesho dhidi ya  Leicester City na michezo mingine sita ya ligi kuu nchini Uingereza katika mwezi February.

Carrick ambaye muda mwingine alikuwa anatumika kama beki wa kati kutokana na matatizo ya majeruhi ya timu hiyo, kuumia kwake ni pigo katika timu hiyo lakini kocha wa timu hiyo Van Gaal amesema kuwa hato sajili mchezaji mwingine katika kipindi hiki cha uhamisho wa wachezaji.

Van Gaal amesema kuwa klabu yake kwa sasa haina mpango wa kununua mchezaji yeyote bali timu hiyo kwa sasa ipo katika mchakato wa kuuza wachezaji amabo wamekuwa hawana nafasi katika kikosi hicho.

Manchester United kesho itashuka dimbani kupambana na Leicester City huku wakiwa na kumbumbuku ya kufungwa goli 5-3 na timu hiyo mwezi September mwaka jana katika mechi ya ligi kuu nchini humo.

 

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!