Searching...
Image and video hosting by TinyPic
22 February 2015
Sunday, February 22, 2015

Kueleke mechi ya Mbeya City vs Yanga


Na Omary Katanga

Kauli iliyoripotiwa kutolewa na kiongozi wa chama cha Soka mkoani Mbeya ya kwamba Yanga hawawezi kuondoka na pointi 6 kwenye michezo miwili ya Tanzania Prisons na Mbeya City,si ya kuibeza hata kidogo.
Hakuna ubishi kwamba masikio yetu wapenda michezo yamezoea kusikia hujuma kufanywa na watu mbalimbali katika mpira,yaweza kuwa viongozi wavilabu,waamuzi,viongozi wa vyama vya mpira,makocha na hata wachezaji wenyewe.
kwa hili ningependa kuishauri TFF kufuatilia kauli hiyo ya katibu wa chama mbeya,ili kubaini kama kuna ukweli wowote na hatimaye kuchukua hatua kali kukomesha kabisa hujuma michezoni.
ANGALIZO:Tff itakapofanya uchunguzi ni lazima pande zote zihusishwe-isijekuwa Yanga wamedanganya ili kuandaa majibu ya kuwapa mashabiki wao endapo watapoteza mechi dhidi ya Mbeya city,Lakini TFF wakati huo huo iwe makini huenda Yanga wamesema ukweli kuhusu kauli hiyo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!