Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 January 2015
Friday, January 30, 2015

Scholes amkingia kifua Costa.


Na Chikoti Cico

Kiungo wa zamani wa Manchester United Paul Scholes ambaye kwasasa anafanya kazi ya uchambuzi wa soka baada ya kustaafu kucheza mpira wa miguu amemkingia kifua mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa ambaye ameshtakiwa na chama cha soka nchini Uingereza (FA) kwa kumkanyaga Emre Can kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili ya kombe la Capital One Jumanne iliyopita.
Na kutokana na shtaka hilo Costa anaweza kufungiwa kucheza michezo mitatu ya ligi kuu nchini Uingereza na hivyo anatarajiwa kukosekana kwenye mchezo wa Chelsea dhidi ya Manchester City utakaochezwa siku ya Jumamosi.
Pamoja na hasira kali ya Costa na mchezo mbaya alioonyesha kwenye mchezo huo dhidi ya Liverpool Scholes amedai ni vyema mshambuliaji huyo wa Chelsea kuonyeshwa heshima zaidi kwani anachokozwa sana na ni mvumilivu.
Akiandika kwenye kolamu yake ndani ya gazeti la Independent la nchini Uingereza Scholes alisema “kuhusu Diego Costa, ninaona tofauti na wengine. Nafikiri matendo yake yalikuwa chini kabisa kwenye mizani ya hatari na alikuwa kwenye hali ya kuchokozwa sana kulikopitiliza kutoka kwa Martin Skrtel ambaye alimpa wasiwasi kabla ya msimu huu”.
“Mtazamo wangu ni kwamba Costa alipigwa sana na kiuhalisia uvumilivu wake unatakiwa kupendwa katika mengi kama sio hali zote.
Kutokana na adhabu ya mechi tatu ambazo Costa anaweza kukosa kama mashtaka ya FA yatasimama mshambuliaji huyo ambaye ana magoli 17 mpaka sasa kwenye ligi ya Uingereza atakosa michezo ya Chelsea dhidi ya Manchester City, Aston Villa na Everton.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!