Searching...
Image and video hosting by TinyPic
19 January 2015
Monday, January 19, 2015

Ghana na Afrika Kusini zaangukia pua.


Na Chikoti Cico.

Katika mfululizo wa mechi za kombe la Mataifa ya Afrika timu ya Ghana maarufu kama “Black Stars” jana iliangukia pua baada ya kupokea kichapo cha magoli 2-1 toka kwa Senegal maarufu kama “Simba wa Teranga”.

Katika mchezo huo wa kundi C linalojulikana kama “kundi la kifo” Ghana ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli kwenye dakika ya 13 kupitia kwa Andre Ayew aliyefunga goli hilo kwa njia ya penati baada ya Christian Atsu kudondoshwa kwenye eneo la hatari na kipa wa Senegal Coundoul.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinaisha Ghana walikuwa mbele kwa goli hilo moja, kipindi cha pili kilianza kwa kasi na kwenye dakika ya 58 Mame Diouf aliisawazishia timu ya Senegal goli lililoipa nguvu timu hiyo.

Na wakati mchezo ukielekea kumalizikia huku mashabiki wakiamini timu zitagawana alama alikuwa ni Mousa Sow aliyeipatia Senegal goli la pili na la ushindi kwenye mchezo kuwapa Simba wa Teranga alama tatu muhimu.

Vikosi vilikuwa hivi: Ghana XI: R Brimah, H Afful, B Rahman, A Mohammed, Jona Mensah, D Amartey, M Rabiu, EA Badu, C Atsu, A Ayew, J Ayew.

Senegal XI: Coundoul; S Mbodji, P Djilobodji, P Diop, L Sane, C Kouyate, MB Diouf, D Ndoye, S Badji, I Gueye, P Souare.

Kwenye mchezo mwingine wa kundi C kati ya Algeria dhidi ya Afrika ya Kusini maarufu kama Bafana Bafana uliochezwa kwenye uwanja wa Estadio de Mongomo nchini Guinea ya Ikweta uliisha kwa Algeria kushinda kwa magoli 3-1.

Bafana Bafana walikuwa wa kwanza kupata goli kwenye dakika ya 51 ya mchezo kupitia kwa Thuso Phala goli lililoamsha shamrashamra za mashabiki wa timu hiyo lakini kwenye dakika ya 67 Algeria walisawazisha goli hilo baada ya beki wa Bafana Bafana Hlatshwayo kujifunga kwa kuunganisha krosi ya Yacine Brahimi.

Baada ya goli hilo la kusawazisha Algeria walikuja juu na dakika ya 72 Ghoulam aliipatia timu hiyo goli la pili na kuiongezea nguvu zaidi timu hiyo, huku mchezo ukikaribia kuisha Slimani aliihakikishia Algeria ushindi kwa kuipatia goli la tatu kwenye dakika ya 83 ya mchezo.

Hivyo hadi mwisho wa mchezo huo Algeria walitoka kifua mbele kwa magoli 3-1 na kuongoza kwenye msimamo wa kundi C.

Vikosi vilikuwa hivi: Algeria: M'Bolhi; Mandi, Medjani, Halliche, Ghoulam, Feghouli, Bentaleb, Lacen (Taider 64'), Mahrez (Belfodil 60'), Brahimi (Soudani 90'), Slimani

South Africa: Keet; Ngcongca, Hlatshwayo, Coetzee (Nhlapo 30'),Furman, Jali, Manyisa, Phala, Vilakazi (Masango 85'), Rantie, (Ndulula 79')

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!