Searching...
Image and video hosting by TinyPic
13 December 2014
Saturday, December 13, 2014

Unaijua Chelsea au Unaisikia?


Na Chikoti Cico

Vinara wa ligi kuu nchini Uingereza timu ya Chelsea imeendelea kujikita kileleni mwa ligi kuu nchini humo baada ya kupata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Hull City katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge majira ya 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki hivyo kufikisha alama 39.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku kila timu ikitafuta goli la mapema lakini walikuwa ni wenyeji timu ya Chelsea waliofanikiwa kupata goli kwenye dakika ya saba kupitia kwa Eden Hazard akiunganisha kwa kichwa krosi iliyochongwa na Oscar Dos Santos hivyo kuiandikia Chelsea goli la kwanza.

Mchezo uliendelea kwa Hull City kutafuta goli la kusawazisha lakini dakika ya 10 ya mchezo beki mahiri wa timu hiyo Michael Dawson aliumia na nafasi yake kuchukuliwa na Bruce, ingawa kila timu iliendelea kutafuta goli lakini mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinaisha matokeo yalibaki kuwa 1-0.

Kipindi cha pili kilianza tena kwa kasi huku Chelsea wakionekana dhahiri kumkosa kiungo wao Cesc Fabregas aliyekuwa anatumikia adhabu ya kutokucheza mchezo huo hasa kwenye kuifanya timu ishambulie na upigaji wa pasi za mwisho hivyo Chelsea pamoja na kumiliki mpira muda mrefu hawakuwa na hatari sana langoni mwa Hull City.

Na kwenye dakika ya 60 kiungo wa Hull City Tom Huddlestone alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya beki wa kushoto wa Chelsea Felipe Luis na dakika saba baadaye Chelsea waliandika bao la pili kupitia kwa Diego Costa baada ya kupokea pasi kutoka kwa Eden Hazard.

Baada ya kadi nyekundu hiyo na goli la pili la Chelsea Hull City walionekana kuzidiwa na hivyo Chelsea kuendelea kutawala sehemu kubwa ya mchezo kuingia kwa Brady na Ramirez bado hakukubadilisha chochote kwa upande wa Hull huku kocha Jose Mourinho akiwaingiza Didier Drogba, Schurrle na Ramirez kumalizia mchezo huo.

Hivyo mpaka mwamuzi wa mchezo huo Chris Foy anapuliza kipenga kumaliza mchezo kwenye dakika ya 93 Chelsea waliondoka uwanjani na alama tatu muhimu huku Eden Hazard akiwa nyota wa mchezo huo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!