Searching...
Image and video hosting by TinyPic
13 December 2014
Saturday, December 13, 2014

Manchester City yang’aa ugenini.


Na Chikoti Cico

Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Uingereza timu ya Manchester City imeendelea kuikimbiza timu ya Chelsea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Leicester City katika mchezo uliopigwa kwenye wa King Power Stadium.

Goli la dakika ya 40 lililofungwa na Frank Lampard baada ya kupokea pasi kutoka kwa Samir Nasri liliihakikishia Manchester City kuondoka na alama tatu muhimu nyumbani kwa Leicester City na hivyo kufikisha alama 36 huku wakiendelea kushika nafasi ya pili.

Haukuwa mchezo mrahisi kwa Manchester City kwani tokea kipindi cha kwanza walikutana na upinzani toka kwa Leicester City ambao walionyesha ari ya kutafuta ushindi huku Vardy, Cambiasso na Schlupp wakiongoza mashambulizi ya timu hiyo langoni mwa Manchester City.

Pia kutokana na uchovu wa wachezaji wa Manchester ambao walicheza katikati ya wiki kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Roma ulichangia kwa timu hiyo kutokuonyesha kiwango kizuri.

Pamoja na mabadiliko yaliyofanywa na timu zote mbili huku Leicester wakiwaingiza Knockaert, Ulloa na Powell huku Manchester City wakiwaingiza Demichelis, Milner na Navas.

Kwa pande zote mbili, hakuna mabadiliko yaliyozaa matunda huku vijana wa Manuel Pellegrini timu ya Manchester City ikifanya kazi ya kulinda goli lao moja na Leicester City wakibaki kujaribu kusawazisha bila mafanikio.

Kwenye mchezo huo mshambuliaji wa Manchester City Edin Dzeko aliumia mapema zaidi wakati wa mazoezi ya kupasha mwili joto na nafasi yake kuchukuliwa na Jose Angel Pozo lakini pia dakika ya 77 nahodha wa timu hiyo Vicent Kompany aliumia na kutolewa nje nafasi iliyochukuliwa na Demichelis.

Mwamuzi wa mchezo huo Jon Moss aliwaonyesha kadi za njano Samir Nasri na Joe Hart wa Manchester City huku kukiwa hakuna mchezaji yeyote wa Leicester City aliyeonyeshwa kadi na mpaka mwamuzi huyo anapuliza kipenga kumaliza mchezo huo matokeo yalibaki Leicester City 0-1 Manchester City.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!