Searching...
Image and video hosting by TinyPic
26 October 2014
Sunday, October 26, 2014

Barcelona wakajipange upya.


Na Rossa Kabwine

Real Madrid au timu ya kifalme, jana waliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wapinzani wao, timu ya Barcelona kwenye mchezo wa kwanza wa El-Classico uliopigwa kwenye dimba la Bernabeu.

Mechi hiyo ilishuhudia kurudi dimbani kwa mshambuliaji, Luiz Suarez ambaye alikuwa nje ya soka la ushindani kwa miezi minne. Suarez alikuwa sehemu ya washambuliaji watatu wa Barcelona walionza jana na, alifanikiwa kutoa pasi ya mwisho ya goli pekee lililofungwa na Neymar Jr.

Barcelona walianza mchezo kwa kasi huku Andres Iniesta na Xaiv Hernandez wakianza sehemu ya kiungo sambamba na Sergio Busquets huku watu wengi wakihoji kitendo cha beki wa kushoto Jordi Alba na Kiungo Ivan Rakitic kupigwa benchi. 

Magoli ya Real Madrid yalifungwa na Christiano Ronaldo ambaye alifunga kwa mkwaju wa penalty baada ya mlinzi wa Barcelona, Gerrard Pique kuunawa mpira eneo la hatari.

Pepe alifunga goli la kichwa na kuwapa uongozi Real Mdarid kabla ya Benzema kufunga goli la tatu. Real Madrid walishangilia ushindi huo kwa sababu umesaidia kupunguza pengo la pointi kati yao na vinara Barcelona.

Real Madrid walionekana kuwa na kasi na kutawala dimba la kati kwa kuwatumia Ton Kross, Luke Modric na Isco huku upande wa ushambuliaji, James Rodriguez, Ronaldo na Benzema wakiwakilisha.

Barcelona mbayo ilikuwa imecheza michezo minane ya La Liga bila kufungwa hata goli moja, jana walikuwa kwenye hali ngumu na hiyo ni kutokana na viungo wake wa kati kuzidiwa ujanja na watoto wa Real Madrid.

Christiano Ronaldo ameendelea kuwa kinara wa magoli huku jana akifikisha goli lake la 13 kwenye msimu huu, huku Karim Benzema akifikisha goli la nne sawa na Gareth Bale ambaye aliukosa mchezo huo wa jana.

Kwa upande wa Barcelona, ujio wa Luis Suarez utawanufaisha kutokana na namna anavyojua kupambana huku muunganiko wa Messi mwenye magoli saba na Nermay aliyefunga magoli tisa mpaka sasa, unaonekana kuwaimarisha Barcelona.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!