Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 March 2014
Friday, March 28, 2014

EDISON CAVAN AIKANA MAN UNITED.IMEKUWA ikiripotiwa kuwa mabingwa watetezi wa ligi kuu Uingereza,klabu ya Manchester United inajiandaa kumnyakuwa mshambuliaji raia wa Uruguay Edson Cavan ambaye amekuwa hapati nafasi kubwa ya kuanza kwenye nafasi ya mshabuliaji wa mwisho tangu kujiunga na PSG akitokea klabu ya Napol ya nchini Italia.

Ingawa alipoulizwa na wanahabari mchezaji huyo kama anaweza kujiunga na man united siku ya ijumaa jioni alijibu kuwa "Mimi ni mchezaji wa Paris Saint German"


Cavan alizungumza na wanahabari baada ya kumalizika kwa mechi yao jana dhidi ya Nice ambapo walifanikiwa kushinda kwa bao 1-0 la utata lililotokana na mpira wa kujifunga wa Timothee Kolodziejczak.

Mshambuliaji huyo aliweza kukiri wazi kuwa vijana hao wa Laurent Blanc hawakucheza vizuri kwenye mchezo huo lakini,alisema kuwa wameuchukulia mchezo huo kama kupasha misuli yao kuelekea mchezo wao na chelsea wa ligi ya mabingwa Ulaya ambapo wanahitaji ushindi.


"Kitu cha msingi nikuona tumeweza kuibuka na ushindi,hayo ndiyo matokeo mazuri kwetu" alisema Cavan.
"Ilikuwa ni muhimu kushinda leo kwa ajili ya kutwaa ubingwa lakini kwa ajili pia ya kujiandaa na mechi yetu dhidi ya Chelsea inayotukabili."

Ushindi wa PSG dhidi ya Nice,watakuwa wanaongoza kwa alama  13 dhidi ya wanaoshika nafasi ya pili timu ya Monaco kwenye msimamo wa Ligue 1.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!