Searching...
Image and video hosting by TinyPic
17 December 2014
Wednesday, December 17, 2014

Falcao atamani kuendelea kukipiga na Manchester United
Na Florence George


Mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia Radamel Falcao ambaye yupo kwa mkopo wa mwaka mmoja  katika kikosi cha Manchester United amesema kuwa anataka kuendelea kukipiga katika timu hiyo yenye maskani yake katika dimba la Old Trafford ikitegemeana amecheza muda gani katika timu hiyo na kwa kiasi gani timu hiyo inamuhitaji.

Mchezaji huyo amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara na kutokuwa katika kiwango cha juu tangu alipotua katika timu hiyo.Tangu mwezi October Falcao ameanza mechi tatu tu za ligi  kuu nchini Uingereza huku akifunga goli moja tu hadi sasa.

Kabla ya mechi dhidi ya Liverpool siku ya jumapili Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal alisema kuwa Falcao alikuwa fiti kuanza mechi ile lakini mchezaji huyo aliingia akitokea benchi dakika 12 kabla ya mchezo kuisha kuchukua nafasi ya Wayne Rooney.

United wananafasi ya kumsajili moja kwa moja mshambuliaji huyo majira ya joto mwakani ambapo bado wanasubiri kumuangalia mchezaji huyo kama atarudi katika  kiwango chake cha awali au la.

Mchezaji huyo amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara ambapo mwezi January aliumia kifundo cha mguu kilichosababisha akose fainali za kombe la dunia Nchini Brazil.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!