Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 December 2014
Tuesday, December 09, 2014

Liverpool safari ya Ueropa League imewadia.




 Na Oscar Oscar Jr

Hatimaye mabingwa mara tano wa klabu bingwa Ulaya timu ya Liverpool, wameweza kuondolewa kwenye michuano hiyo baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Fc Basel kwenye mchezo wa mwisho uliopigwa kwenye dimba la Anfield na sasa, Liverpool watalazimika kwenda kucheza Europe League.

Liverpool hawakuanza kampeni zao vema kwani wamefanikiwa kushinda mchezo mmoja tu kati ya mechi sita za kundi B na kujikuta wakiambualia nafasi ya tatu kwenye kundi hilo.

Kwa upande wa pili, kundi hilo limeshuhudia Mabingwa watetezi wa kombe hilo, Real Madrid wakifuzu kwa kuongoza kundi huku wakifuatiwa na timu ya Basel iliyokamata nafasi ya pili.

Real Madrid wanashika nafasi ya kwanza baaada ya kushinda mechi zao zote sita na kujikusanyia alama 18 huku Basel wao wakishinda mechi zao mbili na kutoka sare mchezo mmoja na kupoteza mechi tatu, wanakamata nafasi ya pili wakiwa na alama saba.

Liverpool wanakamata nafasi ya tatu wakiwa na alama tano huku vibonde kutoka Bulgaria, timu ya Ludogorets wao wakishika nafasi ya mwisho kwenye kundi hilo baada ya kujikusanyia alama nne pekee huku wakishinda mchezo mmoja na kutoka sare mara moja.

Kuondoka kwa mshambuliaji Luiz Suarez aliyekwenda Barcelona, Majeruhi ya Daniel Sturridge na Mario Balotelli yameendelea kuigharimu Liverpool.

Wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu pia, bado hakuna aliyeonyesha kiwango kizuri mpaka sasa huku kipa wa timu hiyo, Simon Mignolet akionekana kufanya makosa mengi yanayoendelea kuigharimu timu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!