Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 December 2014
Saturday, December 20, 2014

King Kibaden arudi Simba.




Na Oscar Oscar Jr

Baada ya kuonekana kana kwamba hakuna mahusiano mazuri kati ya Uongozi mpya wa timu ya Simba, wachezaji wa zamanina na baadhi ya wanachama, mambo yanaonekana kuwa shwari kwa sasa.

Kundi linalojulikana kama Simba UKAWA, wachezaji na viongozi wa zamani wa timu hiyo, wamekubali kushikana na kuhakikisha Simba inasonga mbele.

Rais wa Simba, Evance Aveva kwa kushirikiana na viongozi wengine, wameamua kuwarudisha kwenye kamati mbalimbali, Abdallah King Kibaden na Dua Said huku kundi la tawi la Mpira na Maendeleo nalo likionekana kurejea kambini ili kuitengeneza Simba imara itakayoweza kurudisha heshima iliyoanza kupotea.

King Kibadeni kwa sasa amekuwa makamu mwenyekiti wa kamati ya Ufundi ya Simba huku George Lucas na Dua Said wakiteuliwa kuwa wajumbe. 

Simba wanakamata nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu ambayo ilisimama baada ya kuchezwa mechi saba pekee baada ya kushinda mchezo mmoja na kutoka sare kwenye michezo sita.

Desemba 26 wana Msimbazi hao watakuwa Uwanja wa Taifa kukabiliana na timu ya Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera ambao mpaka sasa wanakamata nafasi ya tano wakiwa na alama 10.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!