Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 December 2014
Saturday, December 20, 2014

Hatimaye ndoto ya klabu ya Simba itatimia.


Na Oscar Oscar Jr

Baada ya uvumi wa muda mrefu sasa kuna matumaini kwa wana Msimbazi kujipatia Uwanja wao. Simba ni moja ya timu kongwe hapa nchini lakini tatizo la kukosa Uwanja wake hata wa mazoezi limeendelea kuchafua taswira yao na sasa kitendawili hicho kinaelekea kuteguliwa.

Taarifa zilizotufikia zinadai kwamba, Bilioni 2.5 zinatosha kabisa kutatua kitendawili hicho ambapo Simba wamepanga kujipatia viwanja viwili na Hosteli za wachezaji kwenye eneo lao la Hekari 19 maeneo ya Bunju, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Ujenzi huo hapo awali ulianzisha na aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage huku akishirikiana na aliyekuwa katibu mkuu wa timu hiyo, Ezekiel Kamwaga lakini baada ya Uongozi mpya kuingia madarakani, kila kitu kilionekana kwenda kombo.

Uwanja huo ambao ulikuwa tayari umeanza kuoteshwa nyasi, uligeuka kuwa machungio ya Mbuzi na mifugo mingine baada ya kukosa usimamizi wa kutosha. 

Uongozi wa Rais Evance Aveva sasa unataka kuhakikisha jambo hilo linamalizika na timu kujipatia uwanja wake. Ramani na tathimini nzima imekamilika na ujenzi unawezaa kuanza muda wowote.

Wapenzi na wanachama wa Simba hawawezi kuridhishwa na ahadi hizo kwani sio mara ya kwanza kutolewa na pengine, kitakacho wafurahisha ni baada ya kuona utekelezaji ukianza.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!