Searching...
Image and video hosting by TinyPic
18 December 2014
Thursday, December 18, 2014

Uche asaini mkataba mpya Villareal CF




Na Florence George


Mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria, Ikechukwu Uche amefanikiwa kuongeza mkataba wa kukipiga katika timu ya manyambizi wa njano Villareal CF inayoshiriki ligi kuu Nchini Hispania.

Sasa mchezaji huyo ataichezea timu hiyo hadi mwaka 2017,huku akiwashukuru viongozi ,wachezaji na hata mashabiki wa timu hiyo kwa ushirikiano wanaompta katika timu hiyo.

Uche ambaye ana umri wa miaka 30 alijiunga na Villareal kwa mkopo akitokea timu ya soka ya Granada inayoshiriki ligi kuu nchini humo mwaka 2011 kabla ya kusajiliwa moja kwa moja na timu hiyo.

Mchezaji huyo alifanikiwa kufunga magoli 14 katika msimu wa 2012/2013,huku akifunga idadi hiyo ya magoli msimu uliopita,hadi hivi sasa mchezaji huyo ameshafunga magoli manne katika mechi 13 alizocheza msimu huu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!