Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 December 2014
Thursday, December 04, 2014

Mbeya City sasa mwendo mdundo.



Na Oscar Oscar Jr

Baada ya vuta nikuvute kati ya Uongozi wa timu ya Mbeya City na kocha wake Juma Mwambusi, hatimaye kila kitu kinaonekana kwenda vizuri na timu hiyo tayari imeondoka jijini Mbeya na kuelekea Songea ambako watapata fursa ya kucheza mechi za kirafiki.

Mbeya City ambao wanaburuza mkia kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara, hivi karibuni ilikuwa katika sintofahamu kufuatia timu hiyo kufanya vibaya kwenye mechi saba za kwanza za ligi na kujikuta wakikamata mkia kwenye msimamo wa ligi kuu.

Kupitia kwenye ukura wa Facebook wa timu hiyo, leo wametoa taarifa kuwa timu hiyo imekwenda Songea na watacheza mechi dhidi ya Majimaji, Jkt Mlale na Mtibwa Sugar na tarehe 10, timu hiyo itarejea Mbeya kuendelea na kambi.

Mbeya City wana alama tano pekee kwenye michezo saba walizocheza mpaka sasa na ligi itakapoanza, watakuwa nyumbani kwenye dimba la Sokoine kuikaribisha timu ya Ndanda Fc kutoka Mtwara.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!