Searching...
Image and video hosting by TinyPic
17 December 2014
Wednesday, December 17, 2014

Xavi afikiria kuwa kocha wa Fc Barcelona




Na Florence George


Mchezaji wa kimataifa wa Hispania na  Nahodha wa Timu ya soka ya Fc Barcelona Xavi Hernandez amesema kuwa anataka kufuata mfano wa Pep Guardiola na siku moja  kuwa kocha wa klabu hiyo.


Kiungo huyo mchezeshaji ambaye ndio namba aliyokuwa anacheza Kocha wa sasa wa Bayern Munich Pep Guardiola alipandishwa katika timu ya kwanza na kocha Louis Van Gaal anayefundisha Manchester United kwa sasa, anafikiria kuwa kocha mara baada ya kustaafu soka lake ndani la klabu yake.

Pep Guardiola alianza kuifundisha Fc Barcelona mwaka 2008 ambapo alifanikiwa kushinda kombe la ligi kuu nchini Hispania mara tatu huku akishinda mara mbili katika kombe la klabu bingwa ulaya katika miaka minne aliyokaa katika timu hiyo.

Xavi anasema kuwa siku za kucheza soka zinahesabika na kurudi katika kiwango chake kama zamani ni ngumu na ni muda wa kupima juhudi alizozifanya katika timu hiyo tangu alipoanza kucheza .

Mchezaji huyo ambaye alistaafu kuichezea timu ya taifa ya Hispania mara baada ya fainali za kombe la dunia Nchini Brazil ambapo timu yake ilifanya vibaya huku ikishindwa kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

 

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!