Searching...
Image and video hosting by TinyPic
17 December 2014
Wednesday, December 17, 2014

Baada ya Maximo, sasa ni zamu ya Manji.



Na Peter Richard Kabita 

 0765178880

Moja ya sifa ya kuu ya wabongo ni kutokua na uvumilivu. uvumilivu hupotea haraka na kusahau yote ya mwanzoni hata kama kuna jambo lolote jema liliofanyika mwanzoni, hakuna atakaye kumbuka. 

Aliyekuwa kocha wa Yanga, Marcio Maximo alipoingia mara ya kwanza Tanzania alipokelewa kwa shangwe kubwa na mashabiki wakiamini kuwa atailetea mafanikio timu yao. 

Maximo mwenyewe alihaidi kuifanyia mambo mazuri yanga. Ili kukiongezea nguvu kikosi cha yanga, akawaleta wachezaji wawili wa kibrazil. Wakwanza, alikuwa ni kiungo Andrey Coutinho ambaye alijazwa sifa za kila aina kwa pasi zake za mazoezini. 

Mwingine ni mshambuliaji mmoja anayeitwa Jaja. Huyu sasa naye akapewa sifa kibao hasa baada ya mechi ile ya Azam kwenye ngao ya jamii kutokana na kufunga magoli mawili. Wana Yanga walimuona kama Mfalme wao!

kawaida yetu ni kukosa uvumilivu. Mechi saba tu zilitosha kuonyesha madudu ya Jaja na wanajangwani hawakuwa na haja naye tena. Magoli yakapotea huku pasi za visigino za Coutinho nazo zikaota mbawa!

Unajua kilichotokea baada ya mtani jembe? Wabrazil vibarua vikaota nyasi. Naamini Manji alitamani kuendelea kumwamini Maximo na kumpa muda zaidi lakini shinikizo la mashabiki na wanachama ndio lilikufanya uchukue maamuzi magumu ya kusitisha ajira ya Maximo.

Ujumbe wangu kwako mheshimiwa Manji, watanzania hatuna uvumilivu, tuna mioyo ambayo haina subira. Wengi bado wanasubiri ahadi yako ya kulipa goli tano ulizoahidi kwa simba.

Kila mnapokutana na Simba, umekuwa mtu wa kuchezea vichapo tu katika uongozi wako. Tunakoelekea kama timu itaendelea kufungwa tu na Simba, hakika kibao kitakugeukia wewe na mashabiki watataka uachie kiti. 

Ni vema ukaanza kusoma alama za nyakati kabla wenye timu mzuka haujawapanda.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!