Searching...
Image and video hosting by TinyPic
17 December 2014
Wednesday, December 17, 2014

Mourinho vs Rodgers kwa mara nyingine tena.


Na Oscar Oscar Jr

Baada ya mechi za robo fainali ya kombe la ligi maarufu kwa jina la Capital One Cup, vinara wa ligi kuu Uingereza timu ya Chelsea sasa watakutana na Liverpool kwenye mchezo wa nusu fainali. 

Utaratibu pia umebadilishwa na sasa kutakuwa na mechi za ugenini na nyumbani ambapo Liverpool wataanzia uwanja wa nyumbani na kumalizia ugenini.

Mechi hizo zimepangwa kuchezwa January 19 mwakani na kurudiwa Januari 26. Mechi ya mwisho iliyowakutanisha Liverpol na Chelsea, ilishuhudia Chelsea wakiibuka wababe kwa ushindi wa mabao 2-1 pale Anfield.

Nusu fainali nyingine itakuwa baina ya Tottenham Hotspurs na Sheffield United kutoka ligi daraja la kwanza. Sheffield United tayari wamekutana na timu za ligi kuu kama Southampton na West Ham na wakaweza kusonga mbele hivyo, mechi dhidi ya Spurs itakuwa ngumu kwa pande zote mbili.

Fainali ya shindano hilo inatarajia kupigwa Machi mosi mwakani. Tottenham wametinga nusu fainali baada ya kuwachapa Newcastle United 4-0 wakati Sheffied United, wao wametinga kwenye hatua hiyo baaada ya kuwalaza Southampton kwa bao 1-0.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!