Searching...
Image and video hosting by TinyPic
13 December 2014
Saturday, December 13, 2014

Uchambuzi: Arsenal vs. Newcastle United


Na Chikoti Cico.

mbalimbali vikitarajiwa kuwaka moto mwisho wa juma hili kwa mechi mbalimbali za ligi kuu nchini Uingereza, timu ya Arsenal wao watakuwa wenyeji wa Newcastle United kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza utakaopigwa kwenye uwanja wa Emirates.

Arsenal wanaoshika nafasi ya sita wakiwa na alama 23 wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Stoke City kwa magoli 3-2 hivyo wanatarajiwa kuingia kwenye mchezo huo kutafuta alama tatu muhimu ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kuingia kwenye “top four”.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger atawakosa Aaron Ramsey, Laurent Koscielny, Nacho Monreal, Mikel Arteta,Theo Walcott, Mesut Ozil,David Ospina, Abou Diaby, na Jack Wilshere ambao ni majeruhi

Pia akimkosa beki wa kati Calum Chambers ambaye anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa kwenye mchezo dhidi ya Stoke hivyo beki wa kulia Mathieu Debuchy ataweza kucheza katikati kwenye mchezo huo.

Kuelekea mchezo huo mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud anaonekana kuwa na rekodi nzuri dhidi ya Newcastle huku akiwa amefunga magoli manne katika mechi nne alizocheza dhidi yao.
Kikosi cha Arsenal kinaweza kuwa hivi: Szczesny; Bellerin, Mertesacker, Debuchy, Gibbs; Ramsey, Flamini; Cazorla, Sanchez, Welbeck; Giroud

Newcastle United kwa upande wao baada ya kushinda mchezo uliopita dhidi ya Chelsea na kupanda mpaka nafasi ya saba wakiwa na alama 23 kwenye msimamo wa ligi wanatarajiwa kuingia kwenye mchezo huo wakiwa ana ari ya kutafuta alama tatu muhimu ili kuendelea kusogea juu zaidi kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Kocha wa Newcastle United Alan Pardew atawakosa Moussa Sissoko na Steven Taylor ambao wamesimamishwa kwa mechi moja pia atamkosa Rolando Aaron ambaye ni majeruhi na atakuwa nje kwa muda wa mwezi mmoja wakati huo nahodha Fabricio Coloccini ataangaliwa kama ataweza kucheza mchezo huo baada ya kuumia.

Newcastle United kuelekea mchezo huo wanaonekana kuwa na rekodi mbovu dhidi ya Arsenal kwani katika michezo 14 iliyopita ya ligi wamefungwa michezo nane, kutoka sare michezo mitano na kushinda mchezo mmoja tu.

Kikosi cha Newcastle United kinaweza kuwa hivi: Alnwick; Janmaat, Coloccini, Dummett; Haidara; Colback, Tiote; Ameobi, Cabella, Perez; Cisse

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!