Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 November 2014
Friday, November 21, 2014

Lionel Messi haendi kokote.



Na Oscar Oscar Jr

Kumekuwa na habari za Staa wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi kutaka kuondoka kwenye klabu hiyo ya nchini Hispania lakini, Rais wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu ameendelea kusisitiza kuwa mchezaji huyo haendi kokote.

Lionel Messi ambaye ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara nne mfululizo, ameendelea kuripotiwa kutaka kuikacha klabu hiyo ambayo imempatia mafanikio makubwa katika maisha yake. 

Rais wa Barcelona amebainisha kuwa, mchezaji huyo anasongwa na mambo mengi ya nje ya uwanja likiwamo lile tukio lake la kupelekwa kwenye vyombo vya sheria kufuatia madai ya kutolipa kodi ya makazi.

Akiongea na kituo cha Televisheni cha 8TV cha Catalunia, Bartomeu amesema kuwa, Messi anaishi kwa furaha sana akiwa Catalunia na hafikirii kama mchezaji huyo ataondoka.

Alipoulizwa Rais huyo juu ya kumpatia Messi mkataba mwingine alijiubu " Hapana hatujazungumzia mkataba mpya ila Messi yuko na furaha hapa" Bartomeu alipata pia nafasi ya kuzungumza na baba wa mchezaji huyo na kusema kuwa, hakuna tatizo lolote.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa zinazohusu mchezaji huyo kuchoshwa na mambo yanavyoendelea kwenye klabu hiyo huku timu kadhaa zikitajwa kumnunua ikiwamo Chelsea ya Uingereza na PSG ya nchini Ufaransa.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!