Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 November 2014
Friday, November 07, 2014

Milioni 14 zawazuzua Stand United


Na Oscar Oscar Jr

Timu ya Stand United imeingia katika mvutano wa Uongozi na Mfadhili wao kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni matumizi mabaya ya fedha. 

Stand Uninted ambayo ina pointi sita tu na kujikuta wakishika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi kuu, wamejikuta kwenye sintofahamu baada ya kupata Milioni 14.

Mechi iliyopigwa kwenye dimba la Kambarage Shinyanga kati yao na timu ya Yanga wiki mbili zilizopita, iliwafanya Stand United kupata mgao wa Milioni 14 na kwa mujibu wa mfadhili wa timu hiyo, Fedha hizo zilipaswa kutumika kulipa madai ya mishahara na usajili wa wachezaji.

Mfadhili wao ambaye anajulikana kwa jina la Fahad Hilal, ameripotiwa kubwaga manyanga kuendelea kuisaidia timu hiyo. Fahad alianza kuisaidia timu hiyo tangu mwaka 2011 na kutokana na kutofautianza na Uongozi wa timu hiyo, ameamua kujiweka pembeni.

Stand United Jumamosi hii, watashuka dimbani Kambarage kumenyana na tiimu ya Mbeya City kutoka mkoani Mbeya. Mbeya City kwa sasa, wanaburuza mkia huku wakiwa na alama tano pekee baada ya kuchezea vichapo mara tatu. 

Stand hawajaonja ladha ya ushindi wakiwa uwanja wa nyumbani na watautumia mchezo huo, kuwapa furaha wakazi wa mkoa huo ambao wanaonekana kuwaunga mkono.

Kutokana na matokeo mabaya ya Mbeya City, Uongozi wa timu hiyo na kocha mkuu Juma Mwambusi, wameendelea kusisitiza kuwa, matokeo wanayopata kwa sasa ni ya mpito tu na hivyo mashabiki na wapenzi wa timu hiyo wasiwe na wasiwasi.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!