Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 June 2013
Friday, June 21, 2013

NIONAVYO MIMI KWA PODOLSKI SIMLAUMU WENGER

                                            

Kuna uwezekana mkubwa sana kocha wa arsenal,arsene wenger aligundua mapema kwamba RVP ataondoka msimu uliopita na ndio maana usajili wa mjerumani Lukas Podolski aliyezaliwa mwaka 1985 ulifanyika mapema sana.
 Bundasliga ni ligi bora ambayo tunaamini inatumia nguvu sana ingawa siku za hivi karibuni inaonekana kubadilika na kucheza mpira wa pasi na nafasi kama Hispania na Brazil ile ya zamani.Ukiniambia Podolski anahitaji kuzoea EPL,mimi sikubali.

wenger alipomsajili LUKAS PODOLSKI wengi tuliamini ni usajili mzuri kwa sababu POLD ananguvu,mbio,uzoefu na yale mashuti yake ya MBAGALA hadi SINZA tukajua wenger amepatia.

PODOLSKI kamuangusha wenger,kwa uwezo wake na uzoefu nadhani angeweza kuziba pengo la RVP.Amemfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi pale EMIRATES lakini amekuwa ni mchezaji ambaye hata kumaliza dk 90 ni mbinde.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!