Searching...
Image and video hosting by TinyPic
25 March 2014
Tuesday, March 25, 2014

YANGA AFRICANS WAKANUSHA TAARIFA ZAKUWA WANABANA BAJETI.

 
 
Young Africans Sports Club yenye makao makuu yake mitaa ya Twiga/Jangwani leo itashuka katika dimba la Uwaja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwakaribisha Maafande wa Jeshi la Magereza timu ya Tanznaia Prisosns ikiwa ni muendelezo wa michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2013/2014.

Kikosi cha Young Africans ambacho kimeweka kambi katika hostali zilizopo makao makuu ya klabu mita ya Twiga/Jangwani asubuhi ya leo  kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola kujiandaa na mchezo huo ambao ni muhimu kwa Yanga kupata ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea Ubingwa wake.

Aidha uongozi unakanusha taarifa zilizotolewa na mwandishi mmoja wa habari kwamba timu imeamua kuweka kambi klabuni ili kubana bajeti hazina ukweli, safari ya kutoka Tabora ni zaidi ya masaa 15 hivyo timu ilifika usiku na becnhi la ufundi wakapendekeza kwa kuwa zimebaki siku mbili kabla ya mchezo ni vyema timu ikakaa klabu kwani kwenda Bagamoyo kwa siku moja ingekua ni kuwachosha wachezaji.
 
Baada ya maombi hayo ya benchi la ufundi uongozi uliridhia na kuandaa kambi makao makuu ya klabu ambapo timu iliingia kambi tangu jana jioni kujiandaa na mchezo huo wa kesho dhidi ya Tanzania Prisons na vijana wote wakionekana kuwa fit kwa mpambano.
 
Kocha mkuu wa Young Africans Hans Van der Pluijm amesema vijana wake wote wapo katika hali nzuri hakuna majeruhi katika kambi, mchezaji pekee atakayeukosa mchezo huo ni Deo Munish "Dida" ambaye alipata majeraha ya kuumia mkono mwishoni mwa wiki na kwa sasa anaendelea na matibabu chini ya usimamizi wa daktari wa timu Dr Suphian Juma.

Kuhusu wachezaji Mbuyu Twite na Didier Kavumbagu walioukosa mchezo wa mwishoni mwa wiki dhidi ya Rhino Rangers mjini Tabora kutokana na kuwa wagonjwa na matatizo binafsi  kwa sasa wako fit na  wameshaungana na timu tangu jana kwenye mazoezi ya jioni  tayari kwa maandalizi na wachezaji wengine kuelekea kwenye mechi hiyo jumatano.

Benchi la Ufundi la Young Africans limesema vijana wao wapo vizuri kwa mchezo wa kesho, morali, kiafya na dhamira ya kupata ushindi ni kubwa hivyo wanaamini kwa jinsi walivyowaandaa vijana watafanya vizuri na kupata ushindi.

Mchezo huo wa kesho unatarajiwa kuanza majira ya saa 10:30 kwa sa za Afrika Mashariki.
 
TAARIFA HII NI KWA MUJIBU WA WEBSITE YA YANGA.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!