Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 November 2014
Thursday, November 20, 2014

Hatimaye Bayern yathibitisha upasuaji.


 Na Oscar Oscar Jr

Hatimaye klabu ya Bayern Munich imethibitisha kukamilika kwa upasuaji wa nahodha wao, Philipp Lahm ambaye aliumia siku ya Jumanne akiwa mazoezini pekee yake bila kuguswa na mtu mwingine. 

Beki huyo amekuwa nguzo kwenye timu ya taifa ambako pamoja na kustaafu, aliiwezesha Ujerumani kutwaa kombe la Dunia nchini Brazil huku, Bayern wakitwaa taji la Bundesliga msimu uliopita chini ya Uongozi wake.

Lamh ni moja ya wachezaji ambao wanajua vema namna ya kutimiza majukumu yao uwanjani licha ya kucheza namba ambazo mara nyingi husababisha wachezaji wengi kupewa kadi, yeye amekuwa tofauti kidogo. Alianza kucheza kama mlinzi wa kulia lakini, siku za karibuni amekuwa akitumika kama kiungo mkabaji.

Kupitia account ya Twitter ya klabu hiyo, wamethibitisha kama nahodha huyo tayari amefanyiwa upasuaji ambao umefanyika kwa mafanikia makubwa na kwa sasa amepewa wiki kadhaa za mapumziko. Lahm huenda akawa nje ya dimba kwa miezi mitatu.

Bayern Munich kwa sasa wanaongoza ligi kuu ya Bundesliga wakiwa na alama 27 ambapo klabu ya Wolfsburg inawafukuzia kwa karibu  wakiwa nafasi ya pili huku wakijikusanyia alama 23 kutokana na timu zote kushuka dimbani mara 11.

Siku ya Jumamosi hii majira ya saa 11:30 Jioni ndani ya Allianz Arena, Bayern watawakaribisha Hoffenheim kwenye muendelezo wa Bundesliga. 

Hoffenheim wako kwenye nafasi ya tano wakiwa na pointi 17 watajaribu kutibua mbio za Bayern Munich ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja msimu huu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!