Searching...
Image and video hosting by TinyPic
24 November 2014
Monday, November 24, 2014

Brendan Rodgers akalia kuti kavu Liverpool


Na Oscar Oscar Jr

Baaada ya kipigo cha jana kutoka kwa vijana wa Crystal Palace cha mabao 3-1, Kocha wa Liverpol, Brendan Rodgers amekiri kuwa kwa sasa amekalia kuti kavu. Hiki ni kipigo cha nne mfululizo kwenye mashindano mbali mbali Liverpool wanayoshiriki msimu huu.

Kichapo hicho kimeifanya timu ya Liverpool kushuka mpaka nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi kuu huku ikiwa na tofauti ya pointi tano baina yao na Manchester United ambao wanakamata nafasi ya nne mpaka sasa baada ya kufikisha alama 19 pale walipowafunga Arsenal kwa bao 2-1 dimbani Emirates.

Siku ya Jumatano ya wiki hii, Liverpool watakuwa na mtihani mwingine wa kushinda mchezo wao wa klabu bingwa Ulaya dhidi ya Ludogorets mabingwa hao wa nchini Bulgaria. 

Brendan Rodgers alipouulizwa juu ya uhakika wa kuendelea kubaki katika klabu hiyo, aliweka wazi kuwa hawezi kuwa na uhakika wakati timu haifanyi vizuri.

Liverpool ambao msimu uliopita walimaliza kwenye nafasi ya pili, msimu huu wanaonekana kusua sua huku kukiwa hakuna hata idara moja kati ya Ulinzi, Kiungo na Ushambuliaji inayoonekana kufanya vizuri. 

Kipigo chao cha jana kimeendelea kudhihirisha ubovu wa safu ya Ulinzi ya timu hiyo ambayo hata msimu uliopita ndiyo iliyochangia kuwanyima ubingwa.

Mchezo wa jana ulishuhudia mshambuliaji Rickie Lambert akianza na kufunga bao la kuongoza kwa Liverpool kwenye dakika ya pili tu ya mchezo. 

Lambert amekuwa akitajwa na wachambuzi wa soka Uingereza kama mtu mwenye uwezo wa kucheza sambamba na Mario Balotelli na kupata mafanikio lakini, Rodgers ameshindwa kumpa nafasi.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!