Namna anavyojichanganya Marcio Maximo.
Na Samuel Samuel
Marcio Maximo kocha wa timu ya Yanga yenye maskani katika mitaa ya Twiga na Jangwani, jijini Dar Es Salaam kuna vitu muhitaji anapaswa kuvizingatia kabla ya kuleta wachezaji toka nchini kwao, Brazil kuja kuchezea timu hiyo inayoshiriki ligi kuu Tanzania na baadae mwakani kombe la Shirikishobarani Afrika.
Maximo ambaye ameingia mkataba wa miaka miwili na wababe hao wa ligi kuu msimu wa 2012-13, kabla ya kuanza kuinoa timu hiyo August mwaka huu , alitua nchini na kiungo mshambuliaji Andrey Coutinho (7) na baadae alimsajili mshambuliaji wa kati toka nchini kwao Geilson Santana " Jaja".
Maximo ambaye kabla ya kutua YANGA, aliwahi kuifundisha timu ya TAIFA ya Tanzania " T stars" kwa mafanikio kiasi hasa kurudisha morali ya watanzania kwa timu yao na kupandisha vipaji vya baadhi ya wachezaji kama Tegete, Kiggy Makasi na Erasto Nyoni.
Katika kazi yake ya kuinoa taifa stars mara nyingi alikuwa akilalamikia kukosa mshambuliaji mzuri wa kati.(9). Mwaikimba ambaye muda huo alikuwa akiichezea Yanga na kulalamikiwa kukosa wepesi lakini bado Maximo aliendelea kumtumia kutokana kasumba aliyonayo juu ya washambuliaji warefu na wasiokuwa na mambo mengi wanapotakiwa kumalizia pasi za mwisho.
Hivyo basi Mbrazil huyo aliondoka nchini akiwa na taswira kwamba nchi hii haina mfumo mzuri wa kutengeneza washambuliaji wa kati hali hiyo imemfanya Maximo asiitendee haki Yanga na wachezaji hao aliokuja nao .
Toka kocha huyo aiche Stars , mpira wa Tanzania umebadilika sana. Maximo ilimpasa kutumia wachezaji aliowakuta na kutathimini uwezo wao kabla ya kusajili mchezaji ambaye mwisho wa siku kaamua kujiondoa mwenyewe baada ya kushindwa kuendana na aina ya soka la Tanzania na mfumo mama wa wachezaji wa Yanga hasa viungo wa pembeni ambao wameonekana wana kasi kuliko yeye .
Maximo kabla ya kumpa majukumu ya mshambuliaji wa kati kijana Jaja , ilimpasa kujua uwezo wa timu hiyo katika nafasi hiyo katika msimu uliopita. Msimu wa 2013-14 nafasi hiyo ilitawaliwa na wachezaji Didier Kavumbagu ambaye alitupia magoli 11, Hamisi Kiiza akifunga magoli 12 huku Mrisho Ngassa akifunga mabao 13.
Hapo kiufundi Maximo alitakiwa kuchukua CDs za Kavumbagu ambaye kama namba tisa alikonga nyoyo za wana Yanga na kulinganisha uwezo wa Jaja kabla ya kumruhusu mchezaji huyo kumwaga wino Jangwani. Kingine ilimpasa kujua uwezo wa viungo washambuliaji kama Ngasa, Kiiza na viungo wa pembeni kama Nizar kabla ya kumsainisha Coutinho ambaye mpaka sasa bado hajaonesha kupata namba ya kudumu na kuiletea mafanikio Yanga kama walivyo fanya Kiiza na Ngasa msimu uliopita.
Kulazimisha kufanikiwa amejikuta kama kocha anatengeneza mifumo ambayo itawalazimisha wachezaji wote wa Yanga kucheza mpira ambao utawafanya Coutinho na Jaja ( kajiondoa kwa sasa) kucheza lakini bado imempa mafanikio madogo sana na kuzua maswali mengi ya kiufundi.
Mbali na hilo, Maximo ameshindwa kutumia ufundi wa wachezaji wengine kama Niyonzima, Kiiza, Hamisi Thabiti, Ngasa ambaye mpaka sasa hana goli hata moja na mkongwe Bahanuzi.
Yawezekana somo limemwingia kocha huyo na tunasubiri kuona usajili mwingine unaomuhusu kiungo mwingine kutoka Brazil ambaye anatarajia kuwasili leo kama utakuwa na tija. 0652464525 .
0 comments:
Post a Comment