Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 December 2014
Saturday, December 20, 2014

Uchambuzi: Aston Villa vs Manchester United


Na Chikoti Cico

Viwanja mbalimbali vitawaka moto kwenye ligi kuu nchini Uingereza huku kwenye uwanja wa Villa Park wenyeji Aston Villa wataikaribisha timu ya Manchester United katika mtanange unaotarajiwa kuwa wa piga nikupige huku kila timu ikitafuta ushindi na kujiweka vizuri kwenye msimamo wa ligi.

Kocha wa Aston, Villa Paul Lambert kuelekea mchezo huo atawakosa wachezaji wake watatu waliosimamishawa ambao ni Alan Hutton, Kieran Richardson na Tom Cleverley ambae hatakama angekuwa hajasimamishwa asingeweza kucheza dhidi ya timu yake kwakuwa yuko kwa mkopo Villa akitokea Manchester United.

Pia kocha huyo atawakosa Ashley Westwood, Joe Cole, Philippe Senderos na Nathan Baker ambao ni majeruhi lakini nahodha Ron Vlaar na kiungo Fabian Delph ambao walikuwa ni majeruhi wanatarajiwa kucheza mchezo huo baada ya kupona.

Kuelekea mchezo huo takwimu zinaonyesha Aston Villa wana rekodi mbaya dhidi ya Manchester United kwenye uwanja wa Villa Park kwani katika michezo 18 iliyopita ya ligi wamefungwa michezo 12 na kutoka sare michezo sita huku wakiwa hawajashinda mchezo hata mmoja.

Kikosi cha Aston Villa kinaweza kuwa hivi: Guzan, Lowton, Okore, Clark, Cissokho, Sanchez, Delph, N'Zogbia, Weimann, Agbonlahor, Benteke.

Kwa upande wa Manchester United kocha wa timu hiyo Luis van Gaal atawakosa Maroune Fellaini, Luke Shaw, Daley Blind, Chris Smalling na Marcos Rojo ambao ni majeruhi ila winga mwenye kasi Angel Di Maria ambaye alikuwa majeruhi anaweza kurejea kwenye mchezo huo huku mshambuliaji Radamel Falcao akikaribia kuwa fiti kabisa.

Baada ya kushinda michezo sita mfululizo na kufikisha alama 31 huku ikishika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi timu ya Manchester United inatarajiwa kuingia kwenye mchezo huo ikiwa na ari ya kuendelea kuwafukuzia Chelsea na Manchester City zinazoshika nafasi ya kwanza na ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney anaonekana kuwa na rekodi nzuri ya kuifunga Villa kuliko timu nyingine yoyote kwenye ligi ya Uingereza mpaka sasa ameifunga magoli 12 huku pia mshambuliaji wa United, Robin van Persie akiwa na rekodi nzuri ya magoli dhidi ya Villa kwani amefunga magoli matano katika michezo mitano iliyopita dhidi yao.

Kikosi cha Manchester United kinaweza kuwa hivi: De Gea; Valencia, Jones, Evans, Young; Carrick, Fellaini, Mata, Rooney; van Persie, Wilson

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!