Spurs wamejiongezea kazi nyingine.
Na Oscar Oscar Jr
Mchezo baina ya Spurs na Burnley umemalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu baada ya kufungana bao 1-1 na sasa watalazimika kucheza mchezo mwingine ili kuweza kupata timu ambayo itakuja kupambana na Leicester City kwenye mzunguko wa nne wa kombe la FA.
Matokeo haya yanawafanya Spurs kucheza mchezo wao wa saba pasipo kupoteza na hali hii inaongeza hali ya kujiamini kwa wachezaji na benchi la ufundi hasa ukizingatia kuwa Spurs walianza kwa mwendo wa kusua sua tangu ujio wa kocha mpra Mouricio Pochettino.
Katika mchezo huo ambao Spurs waliweza kupata asilimia 52 za umiliki wa mpira, walikuwa wa kwanza kujipatia bao kupitia kwa Nacer Chadli ambaye alikuwa akifunga bao lake la tisa msimu huu kabla ya Sam Vokes wa Burnely kusawazisha bao hilo.
Kitendo cha Spurs kushindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa leo ni kama kujiwekea mlima ambao watatakiwa kuupanda kwa kucheza mchezo mwingine hasa ukizingatia kuwa wachezaji wametoka kwenye msimu wa sikukuu ambao kawaida hujuisha michezo mingi ndani ya muda mfupi.
0 comments:
Post a Comment