Searching...
Image and video hosting by TinyPic
25 March 2014
Tuesday, March 25, 2014

BAYERN MUNICH WATWAA UBINGWA WA BUNDESLIGA.



Watoto wa kocha Muhispania klabu ya Bayern Munich imetwaa taji la Ligi Kuu ya Ujerumani, maarufu kama Bundesliga kwa kuweka rekodi baada ya kuifunga Hertha Berlin mabao 3-1 usiku wa jumanne mjini Berlin.Bayern wamechukuwa ndoo yao huku wakionyesha kiwango cha juu kama ambavyo ilitarajiwa na wengi.
Kocha Pep Guardiola ambaye ni kocha wa zamani wa Barcelona, naye ameweka rekodi ya kutwaa ubingwa wa Bundesliga kwa mara ya kwanza na msimu wa kwanza akiwa kocha wa timu.

Mabao ya Bayern katika mechi hiyo yalifungwa na Toni Kroos katika dakika ya 6, Mario Goetze dakika ya 14 na Frank Ribery akamalizia kazi katika dakika ya 79 wakati lile la kufutia machozi lilifungwa na Adrian Ramos kwa penalty katika dakika ya 66.

Bayern imetwaa ubingwa huo huku ikiwa na mechi saba mkononi, hali inayoonyesha kuwa ukali wake msimu huu ilimaliza kabisa ushindani wa Ujerumani.

Washindi hao wa mataji matatu msimu uliopita, wamenyakua taji lao la 23 la Bundesliga tangu michuano hiyo ilipoanzishwa mwaka 1963 kwa rekodi ya kushinda mechi 10 mfululizo.
  Hiyo inafanya Bayern Munich inayofundishwa na kocha Pep Guardiola ifikishe mechi 19 jumla za kushinda mfululilizo katika mashindano yote na mechi 52 za ligi kucheza bila kufungwa.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!