Searching...
Image and video hosting by TinyPic
8 June 2013
Saturday, June 08, 2013

TANZANIA YAFUNGWA 2-1 NA MOROCCO


                                         


NIONAVYO MIMI MOROCO VS STARS

Jana tumefungwa 2-1 na waarabu wa moroco sababu ni moja tu,tulicheza chini ya kiwango basi.Goli lao la Penati na kadi nyekundu ya Agrey Moris ni adhabu halali kabisa.sina tatizo na maamuzi hayo ya refa.

Kim Poulsen naye pia alikuwa chini ya kiwango,sub zake zilikuwa kama za mzee wenger.Tulianza kwa mfumo wa 4-3-3 na baada ya kadi nyekundu akabadilisha na kuwa 4-4-1.kumtoa mtu mwenye nguvu na kasi kama Ulimwengu,hapana angemwacha.

Lewandowski wetu Samatta jana hakuwa kwenye fomu,hatumlaumu.Andres Iniesta wetu Kiemba,kama kawa alinikosha sana kuanzia kuuchezea mpira,mpaka goli lenyewe "classic"

Kelvin Dante Yondani alifanya poa sana jamaa,naamini bado tunanafasi ingawa imekuwa finyu ya kwenda Brazil.

Turudi tumfunge Ivory Coast tutatimiza pts 9 na yeye atabaki na 10.Moroco akimfunga Gambia atafikisha 8,kwa hiyo mechi yake na Ivory coast ya mwisho itakuwa ngumu sana na wakidraw kama awali na sisi tukashinda,Tutaongoza kundi au Morocco akimunga Ivory coast.

Rudini watoto wa JK,najua hata nyie mmeumia kwa matokeo ya jana we love you,we appriciate everything you do.Hamjafungwa,tumefungwa sote.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!