Searching...
Image and video hosting by TinyPic
8 June 2013
Saturday, June 08, 2013

TAIFA STARS




NIONAVYO MIMI KWA MASHABIKI

Timu yetu ya Taifa inapigana kila siku kwa nguvu moja,ari na kila kitu kutuwakilisha.Unapoanza kuichukia Taifa Stars eti kwa sababu imefungwa ni "immaturity" katika soka.

Tunatamani tucheze na kufanikiwa kama Hispania,Ujerumani n.k lakini bado hatuna uwezo huo.Kuna magumu mengi wachezaji wetu wanakutana nayo hasa wanapokuwa nje ya nchi,kwa taarifa yako,hakuna timu Duniani ambayo haifungwi.

Tusikubali kuwa watumwa wa kina Falcao,marco Reus na Hummels kila siku,Tuna kina Samatta,Kiemba na Yondani ambao wanatugusa zaidi ya hao wengine ingawa tunakubali wametuzidi uwezo.

Hapa tulipo leo tumepiga hatua,ukichunguza Stars ya kabla ya Maximo,ya maximo na hii ya leo utagundua kwamba tunasonga mbele.

Bado tunanafasi ya kwenda BRAZIL 2014 hata kama ni finyu ipo.mimi na stars wote ni #made in Tanzania.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!