Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 June 2013
Sunday, June 09, 2013

newcastle na zengwe la mdhamini


                                     



Utata umeibuka juu ya jezi mpya za Newcastle kutoka kwa wadhamini wao kutokana na mshambuliaji wake nyota, Papiss Cisse ameshautaarifu uongozi wa klabu hiyo kwamba hatovaa tangazo la Wonga.com.
Mshambuliaji huyo wa Senegal ni muumini safi wa dini ya Kiislamu na aliwataarifu mapema viongozi wa klabu hiyo juu ya kutokuwa tayari kwenda kinyume cha maadili ya dini yake kwa kutangaza biashara za kampuni hiyo ya mikopo.
 

Kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, waumini wa dini hiyo hawaruhusiwi kunufaika au kujinufisha na riba kutoka kwa mtu mwingine. Benki za Kiislamu hazitoi riba.
Wachezaji wenzake CIsse, Cheick Tiote na Hatem Ben Arfa, ambao pia ni Waislamu, nao pia wanaweza kugoma kuvaa jezi hizo.
                                             

Newcastle haiko tayari kuachana na mchezaji huyo na wanaweza wakafanya kama ilivyokuwa kwa mshambuliaji wa zamani wa Tottenham na West Ham, Freddie Kanoute.
Mmali huyo aligoma kuvaa jezi ya nembo ya tovuti ya 888.com alipokuwa Seville miaka kadhaa iliyopita kwa sababu ya kamari. 

Kanoute alishikilia msimamo wake na hakuvaa nembo hiyo kwenye mashindano ya Hispania, ingawa mazoezini alikubali kuvaa.
Baadaye alikubali kuvaa kwa masharti ya kutotumika katika matangazo yoyote ya kibiashara.
Wonga, ambao udhamini wao wa miaka minne unaanza msimu ujao, tayari inakabiliwa na zengwe lingine katika masuala ya utozaji wa riba za mikopo yake.
Inasemekana mmiliki wa klabu hiyo anafikiria kumuuza mshambulizi huyo kwa klabu ya Russia ili asipoteze dili lake hilo nono na Wonga.

Wonga watapunguza pesa watakazoilipa klabu hiyo kama mmoja wa wachezaji hatovaa nembo yao.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!