Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 June 2013
Friday, June 07, 2013

TAIFA STARS KAZI MOJA TU



Hawa ni vijana wa kitanzania ambao kesho watamenyana na Morocco katika mchezo wa kufuzu kombe la dunia 20014.mechi yao ya kwanza ilichezwa jiji Dar es salaam na Morocco walifungwa goli 3-1.matokeo ya ushindi kwa timu ya Taifa ya TANZANIA yatawaweka pazuri na kupigana kufa kupona kuhakikisha wanawafunga Ivory Coast mechi inayofuata.


Watanzania wamejaa imani kubwa kwa vijana wao na huenda mambo yakawa mazuri kwa sababu hata morocco wenyewe wanaonekana kama kupoteza morari ya mechi hiyo.Morocco ni timu ngumu sana ambayo inaweza kuwafunga Tanzania magoli mengi tu lakini kwa kipindi cha hivi karibuni,TAIFA STARS imeweza kuongeza kiwango na kuwafunga CAMEROON,ZAMBIA nyumbani jijini Dar es salaam.

Kocha wa Tanzania KIM POULSEN amewatoa hofu watanzania na kujenga imani kubwa kwa mashabiki kwa matokeo mazuri a,mbayo yamekuwa yakipatikana.Timu imekaa pamoja kwa muda mrefu na vijana wanaonekana kujiandaa vya kutosha na kusaka ushindi tu.

Kutokana na kufanya vizuri kwa TAIFA STARS watu wengi tayari wameshafika katika nchi ya morocco kwa ajili ya kuishangilia timu yao,viongozi mbalimbali wa chama cha soka TANZANIA na viongozi wa serikali wote wako nyuma ya timu kuipa hamasa.Timu imekamilika na kesho kazi ni moja tu,kusaka pointi 3 ingawa waarabu kuwafunga kwao huwa kunamizengwe kibao.

                                    MUNGU IBARIKI TANZANIA

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!