SISI SOTE NI NDUGU
NIONAVYO MIMI SISI SOTE NI NDUGU.
Tunapokuwa kwenye ligi ya ndani tunalalia kwenye simba na Yanga lakini linapokuja swala la TAIFA STARS wote tunaungana na kuwa kitu moja.TAIFA STARS ni yetu sote na tunahaki ya kuungana na kujivunia.
Kenya kuna Gor Mahia na Fc Leopards wakenya wote wako nyuma ya hizi Club lakini linapokuja swala la HARAMBEE STARS wanaungana wote kuipa nguvu timu yao na kuweka siasa zao pembeni.Hii ndo faida ya soka,kuunganisha watu.
Mwaka 2010 kule nchini Africa kusini,kila mwafika alikuwa nyuma ya timu ya Ghana na Suarez aliwaudhi sio waGhana tu ni waafrica wote.Kumbe sisi ni wamoja na ni ndugu.
Kama Stars itafanya vizuri,Nchi zote za Africa mashariki zitaishabikia kwa sababu sisi ndo majirani zao wa karibu na kama itakwenda BRAZIL Bara zima la Africa litaishangili na kuiunga mkono,SISI SOTE NI NDUGU.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI AFRICA.
0 comments:
Post a Comment