Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 January 2015
Wednesday, January 28, 2015

Figo autaka uraisi wa FIFA.


Na Chikoti Cico

Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Ureno Luis Figo ametangaza nia ya kugombea nafasi ya Uraisi kwenye shirikisho la soka Dunia (FIFA), mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid anaungwa mkono na mashirikisho matano ambayo ni wanachama wa FIFA ikiwa ni mojawapo ya kigezo kinachohitajika kwa mgombea kuingia kwenye kura za mwezi Mei.
Figo anakuwa mchezaji wa zamani wa pili kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho cha kugombea uraisi wa FIFA baada ya mchezaji wa zamani wa Newcastle United na Tottenham Hotspur David Ginola pia kutangaza nia yake ya kutaka kuwa mgombe ingawa bado hajapata mashirikisho matano ya kumuunga mkono.
Kuingia kwa Figo kama mgombea wa uraisi kunamaanisha mpaka sasa kuna wagombea kama wanne kwenye kinyang’anyiro hicho cha uraisi wa FIFA. Mpaka sasa wagombea ni Raisi wa sasa wa FIFA Sepp Blatter na Figo, Mtoto wa Mfalme wa Jordan Ali Bin Al Hussein na Raisi wa chama cha soka cha nchini Uholanzi Michael van Praag wengine ni Mwanadiplomasia wa zamani wa Ufaransa Jerome Champagne ambaye bado hajapata wa kumuunga mkono lakini anaweza kupata.
Figo akiongea na CNN alisema “najali kuhusu soka hivyo ninachokiona kuhusu taswira ya FIFA sio tu sasa lakini tokea miaka iliyopita sikipendi. Kama ukitafuta FIFA kwenye mtandao unaona nen la kwanza linalokuja ni kashfa, sio neno zuri. Ndicho ambacho tunahitajika kukibadilisha kwanza na kujaribu kuboresha taswira ya FIFA”.
“Soka linastahili makubwa zaidi ya hili. Nimekuwa nikizungumza na watu wengi wa muhimu kwenye soka, wachezaji, mameneja, maraisi wa mashirikisho na wote wanafikiri kitu lazima kibadilishwe”. Mabadiliko kwenye uongozi, utawala, uwazi na mshikamano hivyo nafikiri ni muda wa hayo”.
Naye kocha wa Chelsea Jose Mourinho ameonyesha kumuunga mkono Figo akisema “naamini katika mwenendo na mtazamo wake pamoja na mapenzi kwaajili ya mchezo. Atakuwa raisi “atakayefokasi” kwenye soka na maboresho yake kiujumla, akifanya kazi kwa ukaribu na mashirikisho yote”.
Pia kocha wa Southampton Ronaldo Koeman ambaye alimfundisha Figo akiwa Barcelona kwa miaka miwili pia anaamini Figo anaweza kusaidia kuleta mabadiliko FIFA. Alisema “ugombea wa Figo ni nafasi kwaajili ya mabadiliko ya FIFA. Ninamjua binafsi na najua kwamba huu ni uamuzi uliosimamia kwenye hitaji la kutoa mwelekeo mpya kwa taasisi ambayo imekumbwa na uharibifu mkubwa kwa miaka iliyopita”.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!