Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 November 2014
Thursday, November 27, 2014

Ni Steven Gerrard au Chelsea msimu huu?



 Na Abuu Hussein 
0715 765 848. 

Unaikumbuka September 11 mwaka 2003? hii ni siku ambayo wamarekani pamoja na dunia nzima hawataisahau hasa kwa kile kilichowakuta baada ya uratibu mzuri wa kundi la kigaidi la Al-Qaida.

Kundi hili lilifanikuwa kuishambulia marekani katika majengo yake mawili pacha ya pentagoni kwa kutumia ndege zilizogonga majengo hayo mawili na kusababisha mlipuko mkubwa na uliopelekea idadi kubwa ya vifo vya watu pamoja na majeruhii. 

Unajua ni kwanini magaidi wa kundi la Al-Qaida walifanikiwa kuishambulia marekani pamoja na kuwa ndo nchi yenye ulinzi mkali zaidi duniani na inayotumia vifaa vya kisasa zaidi vya ulizi ?, 

jibu ni kuwa Al-Qaida walikuwa na nia ya kufanya shambulizi hilo kwa muda mrefu sana na hivyo iliwabidi wajipange na kutafuta mbinu itakayo wasaidia kutimiza nia yao hiyo ovu ya kuishambulia marekani . 

Zoezi la kwanza kabisa walifanya majaribio ya kulipua balozi za marekani nchini Tanzania na Kenya ambapo walifanikiwa na kuona wanaweza kufanya tukio kama hilo nchini Marekani. 

Ukurasa wa pili wa maisha kuna tukio lingine linalomhusu kijana mmoja nchini Uingereza, katika karia yake ya mchezo wa mpira wa miguu kijana huyu anatamani sana walau aweze kushinda taji la ligi kuu ya England, maarufu kama Barclays premier league, huyu si mwingine ni Steven Gerald nahodha na mpambanaji wa klabu ya Liverpool.

Nafikiri unamtambua vizuri saana na kukukumbuka mambo makubwa aliyokwisha kuifanyia klabu yake ya Liverpool na timu yake ya taifa England. 

Gerald ni mmoja ya watu wanaoishi kwa machungu na maumivu makubwa zaidi katika karia yake ya mchezo wa mpira wa miguu pamoja na kuwa na utajiri mkubwa wa fedha, nyumba,magari ya kifahari, ukiachana na vitega uchumi vingine.

Gerald ndoto yake ni kuchukua taji hilo na timu yake ya Liverpool ambayo ameitumikia kuichezea tokea akiwa mtoto na kufanikiwa kunyakua vikombe vyote vya mashindano kuanzia FA Cup,Carling Cup,Uefa champions league pamoja na Europa league. 

Kuna rekodi kadhaa zimekuwa zikiyatia simanzi maisha ya baadhi ya wachezaji pamoja na mashabiki wa ligi kuu England, mojawapo ikiwa ni ile inayomhusu kiungo Steven Gerald kutochukua taji la ligi kuu Englang.

Kumekuwa na rekodi inayohusu bingwa wa ligi kuu ya England na mshindi wa pili, mmoja kutwaa ubingwa wa ligi hiyo msimu unaofuata tangu msimu wa 2006/2007. Je, Chelsea aliomaliza nafasi ya tatu msimu uliopita ataivunja au Gerrard na Liverpool, watatisha?

Josse Morinho akionekana kuanza vizuri na timu yake ya Chelsea kwa kushinda michezo kumi na kutoka sare michezo miwili huku pia kwenye michuano ya klabu bingwa ulaya akishinda michezo yake yote.

Hii ni kiasi ya timu ilivyopania kuchukua vikombe vya mashindano ya FA Cup, Carling Cup, Uefa champions league pamoja na kikombe cha ligi kuu ya England. 

Pamoja na kuanza kwa speed ya ajabu na kutoa vipigo kwa timu zote kubwa za EPL isipokuwa Manchester united ambayo walitoka sare katika mtanage uliozihusisha timu hizo.

Chelsea wanakabiliwa na mfupa mgumu wa kuuvunja, mfupa huo si mwingine ni ile rekodi iliyodumu kwa misimu tisa sasa inayomhusu bingwa wa ligi kuu ya England na mshindi wa pili wa ligi hiyo ndio mmojawapo huwa anafanikiwa kuchukua ubingwa kwa msimu unaofuata tokea msimu wa mwaka 2006-2007. 

Chelsea msimu wa 2013 – 2014 walimaliza katika nafasi ya tatu huku mabingwa wakiwa ni Manchester city wakifuatiwa na klabu ya Liverpool kwa kushika nafasi ya pili.

Kitendo hiki kinachopelekea Chelsea kuwa na kazi ngumu ya kufanya kuhakikisha wanachukua ubingwa wa ligi kutokana na rekodi kutowapa nafasi ya kuchukua ubingwa msimu huu baada ya msimu uliopita kushika nafasi ya tatu na hivyo Manchester city na Liverpool kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa kwa kubebwa na rekodi hiyo.

Japokuwa  msimu huu timu hizo zimeanza vibaya kwa kupoteza michezo kadhaa na kushindwa kupata pointi dhidi ya timu inayoongoza ligi ambayo ni Chelsea wakiwa na ponti 32 kileleni mwa msimamo wa ligi. 

Pamoja na ugumu wa ligi ya England je? Steven Gerald na Chelsea watafanikiwa kuzivunja rekodi zinazowakabili ?. Nawakilisha kwenu wadau.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!