Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 January 2015
Wednesday, January 28, 2015

Henry aanza kusomea ukocha.

Na Chikoti CicoMshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal Thierry Henry ambaye kwasasa ameajiriwa kama mchambuzi wa soka kwenye kituo cha televisheni cha Skysports ameanza mafunzo ya ukocha baada ya kuamua kustaafu soka mwishoni mwa mwaka uliopita.

Henry ametajwa kuanza kuchukua kozi za ukocha kutoka shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) nchini Wales, mshambuliaji huyo ambaye aliwahi pia kuichezea klabu ya Barcelona ametajwa kufanya kozi ya ukocha kwa leseni ya ngazi B ya UEFA.

Henry alifanya uwasilishaji kwenye kikosi cha Wales  umri  chini ya miaka 16 mapema wiki hii na anatarajiwa kuungana na mchezaji mwenzake wa Arsenal Freddie Ljungberg katika kuchukua kozi hiyo ya ukocha. 

Pia taarifa zinasema Henry mwenye umri wa miaka 37 kama akifaulu inawezekana akakamilisha leseni ya ngazi A kwenye majira ya joto mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!