Searching...
Image and video hosting by TinyPic
26 June 2013
Wednesday, June 26, 2013

NIONAVYO MIMI KWA MPIRA WETU WA TANZANIA



 
Kama mtu anaweza kuniamsha usiku wa manane na kuniambia nipendekeze jina moja la mchezaji wa kizazi hiki Tanzania ambaye anatakiwa kujengewa mnara,bila kutafuna maneno nitamtaja JUMA KASSEJA.

Huyu jamaa anafanya kazi nyingi kwanza ni mchezaji na pili ni kiongozi.Tumeshuhudia viongozi wengi wakiwa sehemu ya mgogoro ila kwa huyu jamaa sijawahi sikia akianzisha mzozo iwe kwenye club yake ya SIMBA au STARS.Anakaribia miaka 10 uwanjani akiwa kwenye kiwango bora kabisa.

KASSEJA ni aina ya mchezaji ambaye SIMBA ikifungwa au STARS,huwa anabaki amejishika kiuno na kukosa raha kabisa huku wengine wakicheka cheka tu!! golikipa anaweza cheza hata akiwa kwenye umri mkubwa kwa sababu hakimbii sana uwanjani.

Kwa mpira wetu wa kibongo,sidhani kama KASSEJA kazeeka.Uwezo wa mchezaji haupimwi kwa umri tu bali uwezo wake uwanjani.kuna uwezekano mkubwa sana Kelvin Yondani,Nadir Harobu,Amri Kiemba,Nizar Halfan,Ngassa n.k wote wakawa zaidi ya umri wa mika 30.Unamkumbuka Peter Manyika?

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!